CCM Yamteua Mtoto wa Celina Kombani Kugombea Ubunge Jimbo la Ulanga

03:36


Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ulanga, kimemchagua mtoto wa kwanza wa aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utumishi), Celina Kombani, Godluck Mtinga kuwania ubunge katika Jimbo la Ulanga Mashariki.

Katibu wa CCM wa wilaya hiyo, Mathias Mbogo alisema Mtinga (pichani) aliibuka kidedea kwa kupata kura 731 kati ya 1,029 zilizopigwa na kupendekezwa kuwania nafasi hiyo iliyokuwa inawaniwa na mama yake aliyefariki dunia Septemba 24, mwaka huu nchini India.

Alisema idadi ya wapigakura waliojitokeza walikuwa 1,029, lakini kura halali zilikuwa 1,025 huku nne zikiharibika. Aliwataja wagombea wengine katika uchaguzi huo kuwa ni Aziz Aziz aliyepata kura 134, Omari Dokodogo kura 52, Augustino aliyepata kura 41, Wenslaus Mkunla kura 39, Faustine Kipau 11, Herieth Mwakifulefule tisa na Daud Kitolelo aliyepata kura nane.

Kwa mujibu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), uchaguzi wa majimbo ya Ulanga Mashariki na Lushoto ulioahirishwa kutokana na vifo vya wagombea utafanyika Novemba 22, mwaka huu.

You Might Also Like

1 comments

  1. Merkur Gold Strike Safety Razor - FEBCASINO
    Merkur's Gold Strike septcasino Safety Razor, https://febcasino.com/review/merit-casino/ Merkur Platinum Edge worrione Plated Finish, German, Gold-Plated, Satin Chrome Finish. 메이저 토토 사이트 Merkur has a more aggressive gri-go.com looking,

    ReplyDelete

Popular Posts

Like us on Facebook

Flickr Images