FeaturedLoading...

WAAMKA KULA DAKU, WAMKUTA NYOKA MWENYE HIRIZI

IMG_5651Nyoka huo baada ya kuuawa.
Dustan Shekidele, Morogoro
Inatisha! Ndani ya Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, familia ya mwanaume aliyetambuliwa kwa jina la Hamis Juma, imekumbwa na mauzauza baada ya kuamka ili kula daku na kukutana na nyoka mwenye hirizi mlangoni.
IMG_5649Mama mwenye nyumba hiyo, Mama Nurdin akitaharuki baada ya kutokea hali hiyo.
Tukio hilo lililozua taharuki lilijiri mapema wiki hii kwenye nyumba ya familia hiyo inayoishi Mtaa wa Mkota Kata ya Kiwanja cha Ndege mjini hapa.
IMG_5668Majirani wakishangaa hali hiyo.
Baada ya kutonywa juu ya tukio hilo, Ijumaa lilifika kwenye familia hiyo alfajiri na kushuhudia nyoka huyo aliyekuwa na hirizi na kitambaa cheusi shingoni akiwa mlangoni.
IMG_5677Akisimulia kisa hicho baba wa familia hiyo, Hamis alisema kuwa waliamka saa 7:00 usiku ili kupata daku kama kawaida kwani walianza kufanya hivyo tangu walipofunga.
“Wakati tukiwa sebuleni tunakula, tulianza kuona damu nzito ikisambaa kutokea mlangoni.
IMG_5678“Ukweli tulishtuka sana. Tulipofungua mlango tulishtuka kuona nyoka mkubwa mlangoni akiwa na hirizi huku damu zikiendelea kusambaa kutoka pale alipokuwa yule nyoka.
“Ilibidi tufunge mlango hadi alfajiri tuliamua kuwaita watu waje kushuhudia na kusaidia kumuondoa,” alisema Hamis.
IMG_5681Diwani wa Kata ya Kiwanja cha Ndege, Mohamed Matikula akimpa pole Mama Nurdin.
Katika kutafuta msaada wa kumuondoa nyoka huyo na kusafisha damu zilizozagaa, alitokea mjomba wa familia hiyo ambaye jina halikupatikana akaanza kumtoa kwa kutumia mti, jambo lililosababisha taharuki kwa watu waliokuwepo wakaanza kukimbia.
Baada ya kumtoa nyoka huyo, watu walianza kumpiga wakitaka kumchoma moto lakini alitokea mwanaume asiyefahamika akamkwapua na kuanza kukimbia naye mitaani.
IMG_5664Wakati akikimbia, kundi la watu lilikuwa likimkimbiza ndipo alimtupa na kutokomea kusikojulika.
Katika hali ya kushtua zaidi, nyoka huyo alibadilika, akawa hana hirizi huku akionekana ‘kadogo’ jambo lililoibua madai ya ushirikina hivyo watu wakamuua.
IMG_5695Baba mwenye nyumba hiyo, Hamis Juma.
Kwa upande wake mke wa Hamis, Mama Nurdin ambaye ni mjumbe wa mtaa huo, alishtushwa na tukio hilo na kusema familia yake imekumbwa na hofu kubwa.
Uongozi wa Kata ya Kiwanja cha Ndege ukiongozwa na Diwani, Mohamed Matikula na Afisia Mtendaji, Diha Zongo walifika eneo la tukio na kuwachukua baba na mama wa familia hiyo hadi ofisi ya kata kwa mahojiano zaidi.

LULU MICHAEL AMWAGA MINOTI

ULE msemo wa ‘pata pesa tuone tabia yako’ huenda ni kweli, kufuatia staa wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael Kimemeta ‘Lulu’ ambaye siku hizi anaitwa ‘tajiri mtoto’ kutokana na kuwa na fedha na kumwaga ‘minoti’ (pesa) kwenye pati, Ijumaa ‘Kubwa’ lilikuwepo.
Staa wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael Kimemeta ‘Lulu’.
Kwa mujibu wa shushushu wetu, ishu nzima ilijiri usiku wa Ijumaa iliyopita kwenye pati ya ‘bethidei’ ya mwanamuziki wa Bendi ya The African Stars ‘Twanga Pepeta’, Kalala Hamza ‘Kalala Junior’ iliyofanyika ndani ya ukumbi wa hoteli moja yenye hadhi ya nyota tano iliyopo Masaki jijini Dar ambapo mastaa na mapedeshee kibao wa ‘mujini’ walihudhuria.
LULU AMWAGA MINOTI
Ilielezwa kwamba, Lulu alifanya ‘kufuru’ hiyo baada ya waalikwa wa pati hiyo kumaliza kula na kunywa ambapo ikafika wakati ratiba ikaelekeza watu kutoa zawadi kwa kadiri watakavyojisikia au kujaliwa nacho.
Ndipo Lulu ambaye siku hizi amekuwa hapendi kujitokeza kwenye shughuli, alipita mbele na kuanza kumpa noti nyekundu ‘Msimbazi’ aliyekuwa akizikusanya kwa niaba ya Kalala Junior kwa staili ya moja-moja.
Elizabeth Michael ‘Lulu’ akihesabu minoti.
Shuhuda wetu alidadavua kuwa, kila aliponyoosha mkono kutoa Msimbazi mmoja, watu walimkodolea macho wakiamini hawezi kufika ‘kilo moja’ (Sh. 100,000).
MANENO YA WATU
“Lulu bwana, anajitutumua tu. Hawezi kumpa laki moja Kalala Junior. Kwanza sidhani kama siku hizi ana pesa za kufanyia fujo,” alisema mwalikwa mmoja, mwenzake akampinga.“Wee! Lulu siku hizi ana pesa. Wenzake wanamuita tajiri mtoto. Ndiyo maana ana jeuri ile,” alisema mwingine miongoni mwa waalikwa hao.
Hata hivyo, Ijumaa halikuweza kufuatilia noti hizo katika mtiririko wa kutoka ili kujua ni shilingi ngapi bali baada ya kumaliza, lilimfuata Lulu ili kumuuliza ambapo hakuwa tayari kutoa ushirikiano.
Mtu wa karibu na Lulu ambaye aliomba jina lihifadhiwe, aliliambia Ijumaa kuwa, Lulu siku hiyo alitenga shilingi milioni moja na laki nne (1,400,000) kwa ajili ya kumtuza Kalala Junior tu.“Hawezi kusema, lakini mimi ninavyojua alitenga milioni moja na laki nne. Lulu kwa sasa yuko vizuri kipesa,” alisema mtu huyo na kuachana na Ijumaa.
KWA NINI LULU ALITOA KIASI HICHO CHA PESA KWA KALALA JUNIOR?
Habari za ndani zinasema kuwa, Lulu aliamua kumwaga mkwanja huo kwa vile, mwanamuziki huyo kwa sasa ni mpenzi wa shoga kipenzi wa Lulu, Rose Alphonce ‘Muna’.
Wakati wa matatizo ya Lulu kuswekwa Magereza ya Segerea, Dar kwa madai ya kumuua bila kukusudia aliyekuwa staa wa filamu Bongo, marehemu Steven Kanumba, Muna ndiye aliyebeba jukumu la kumpelekea chakula mahabusu huyo kila siku.
Lakini pia, Lulu alipotoka gerezani kwa dhamana, alikwenda kuishi kwa muda nyumbani kwa Muna, Mwananyamala jijini Dar.
MAPEDESHEE NAO
Baada ya Lulu kumaliza kutuza minoti yake, mapedeshee waliokuwa ukumbini humo nao walicharuka ambapo walichomoa minoti yao na kuimwaga kwenye maboksi mawili na kutolewa ukumbini hapo na wapambe.
KUMBE KALALA ALIFANYIWA SAPRAIZI
Kwa mujibu wa chanzo chetu ndani ya ukumbi huo, Kalala Junior akiwa hajui chochote, mpenzi wake huyo ambaye pia ni msanii wa filamu, alimtaka watoke kwa ajili ya kupata chakula cha jioni ambapo walikwenda kwenye hoteli hiyo.
Elizabeth Michael ‘Lulu’ akiwa na Kalala Hamza ‘Kalala Junior’.
Baada ya kufika, Kalala alipokelewa na watu waliokuwa ukumbini hapo huku wakimmwagia maji, bia na soda hadi akawa chapachapa huku wakimwimbia nyimbo za ‘hepi bethidei tu yuuu…’ jambo ambalo hakulitegemea.
Kutokana na kulowa chapachapa, Muna  alimchukua hadi kwenye chumba alichochukua mapema ndani ya hoteli hiyo ambapo alimbadilisha nguo.
Muna alimvalisha Kalala suti yenye gharama ya shilingi 2,800,000, viatu vya shilingi 800,000 (inadaiwa ni vya kutoka Italia), vyote hivyo alivinunua mwanadada huyo ikiwa ni zawadi kwa mpenzi wake.
Wawili hao walirudi ukumbini ambako walipokelewa kwa shangwe huku mtangazaji maarufu Bongo, Maimartha Jesse ‘Mai’ akiwa ni mshehereshaji (MC) wa shughuli hiyo ambayo kwa kuangalia tu iligharimu mamilioni ya shilingi.
KALALA AMFUNGUKIA MUNA
Kufuatia mbwembwe hizo za Muna, Kalala alitumia nafasi hiyo kumtambulisha rasmi kwamba ndiye mchumba’ke wa sasa na kumshukuru kwa kumwandalia sherehe kubwa na ya gharama kwani hakuwahi kufanyiwa hapo awali.
MAIMARTHA ATIA NENO
Naye mshereheshaji wa shughuli hiyo, Maimatha aliliambia gazeti hili kwamba, sherehe hiyo ilikuwa ya aina yake na yeye alilipwa zaidi ya shilingi milioni moja

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa ya July 3


Habari  Zilizopo  Katika  Magazeti  ya  Leo  Ijumaa  ya  July  3

BORA WASANII HAWA BUNGENI!

JOTO la Uchaguzi Mkuu linazidi kupanda miongoni mwa wanasiasa kutoka vyama mbalimbali vya kisiasa, huku idadi kubwa ya wasanii wakionesha nia ya kutaka kuitwa waheshimiwa kuanzia mwishoni mwa Oktoba mwaka huu.
Hadi sasa baadhi ya waliotangaza nia ni Joseph Haule (Profesa Jay), Zuwena Mohamed (Shilole), Wema Sepetu, Steve Mengere ‘Steve Nyerere’, Jacob Stephen (JB), Mrisho Mpoto na wengineo kadhaa, wakitaka kwenda kuungana na wenzao Joseph Mbilinyi wa Chadema pamoja na Vicky Kamata kutoka CCM.
Hakuna mwenye uhakika nini hasa kitatokea katika uchaguzi huo, ingawa uwezekano wa wasanii hao kuleta ushindani na hatimaye kushinda ni mkubwa, hasa ukirejea jinsi Sugu alivyoingia pasipo kutarajiwa na wengi. Ingawa waigizaji hawa wamekuwa na mambo kadhaa nje ya uwanja, hilo haliwezi kuwa jambo lenye kutia shaka juu ya uwezekano wao wa kushinda.
Wengi wamekuwa wakipiga picha na kuona taswira ya bunge hilo litakalokuwa na wasanii hawa, kwani huenda likaongeza mvuto na kulifanya kuwa moja kati ya mabunge yatakayotazamwa sana na watu, kwa lengo la kuwasikia tu wanachosema, bila kujali kama kitakuwa cha maana au lah.
Kwa ambao wamekuwa wakifuatilia vikao vingi vya Bunge katika miaka ya karibuni, wameliona kama lililopoteza mwelekeo ambalo linatumia muda mwingi kwa wabunge kurushiana vijembe bila kujali kama mada iliyo mbele yao ina masilahi gani kwa taifa lao.
Wengi wamekuwa wakikerwa na jinsi wabunge wengine wanavyopoteza muda kuzungumza mambo yasiyo na tija kwa taifa na badala yake kuweka mbele sana itikadi ya vyama vyao, hata kama kinachojadiliwa mbele yao ni kitu muhimu kiasi gani kwa nchi yao.
Kwa staili hiyo ya ubunge, wasanii hawa wana nafasi kubwa ya kushinda kupitia vyama vyao, kwani watu wanaona ni bora kuwaona waigizaji orijino wakiigiza bungeni, kuliko wabunge ambao mara nyingi wanaonekana kuwa wasio na mchango mkubwa kwa taifa.
Hata hivyo, hivi ni kweli wasanii hao wamejipima na kujiona wanatosha kuwania ubunge au ni ile janja ya siku hizi ya kutangaza nia ili kuwatia hofu wengine wanaotaka nafasi hiyo?
Maana taarifa ambazo siyo rasmi, zinasema siku hizi watu wengi hutangaza nia makusudi ili kuwapa presha wabunge kwenye majimbo yao, wakiamini kuwa baadaye watafuatwa na ‘kupozwa’ kitu kidogo, kama ambavyo uvumi huo umewahi kuhusishwa na watu kadhaa hapo nyuma.
Kwa sababu katika hali ya kawaida, ni kwa namna gani baadhi ya wasanii hawa, ambao maisha yao yamejaa utata wataweza kupewa kura na wananchi wanaohitaji watu makini wenye kujua matatizo na suluhisho lake?
Siwadharau, lakini siyo vibaya kuwakumbusha kuwa ubunge siyo kitu rahisi kama kupata uongozi wa Bongo Movie au kuwa muigizaji mkuu katika filamu. Ni zaidi ya kuwaimbisha watu katika majukwaa ya muziki yaliyojaa vijana wengi.
Wanapaswa kujua, ubunge unahitaji mtu mwenye uwezo wa kujenga hoja na anayejua wananchi wanahitaji na si vinginevyo.

BREAKING NEWSSS: BUNGE LAHAIRISHWA TENA LEO


Spika wa Bunge Mh Anna Makinda Amelazimika Kuharisha Shuguli za Bunge Mpaka Jioni Mara baada ya Kuzuka Vurugu wakati Wakati waziri wa Niashati na Madini Mh Simbachawene Akiwasilisha Muswada wa Petroli na Gesi Bungeni.Hali Ilikuwa Hivi.'
Muongozoooooooooooooooo!!Wamesikika wabunge wa upinzani na spika kuahirisha bunge wakati waziri wa nishati na madini akisoma muswada wake.Kwa nini hii miswada inalazimishwa kwa nguvu???? 

ESHA BUHETI AKIRI KUCHEPUKA


esha_buheti6Mwigizaji Bongo, Esha Buheti katika pozi.
Na Brighton Masalu
Mwigizaji Bongo, Esha Buheti, licha ya kuwa ndani ya ndoa, amekiri kuchepuka na mcheza mpira mmoja ambaye hakutaka kuweka wazi jina lake.
sher131Akizungumza na Ijumaa, Esha aliweka wazi hisia zake kuwa kwa sasa ana kifaa kipya chenye hadhi na amekuwa akitupia picha zake mitandaoni kisha anazitoa.
“Najua wambeya watataka kumchunguza mpenzi wangu wa sasa ndiyo maana namuweka mtandaoni kisha nafuta harakaharaka,” alisema Esha.
EsheBuhetiEsha alifunguka kuwa, pamoja na ‘kidumu’ alichonacho bado yuko kwenye ndoa yake na anamheshimu mumewe aliyezaa naye mtoto mmoja.

DIAMOND AKIRI KUMPENDA OMOTOLA

Mwandishi wetu
KING wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ametengeneza kichwa cha habari nchini Nigeria baada ya kufunguka kuwa anampenda ‘vibaya’ staa wa filamu nchini humo, Omotola Jalade Ekeinde, Ijumaa lina stori kamili.

WASTARA ATAJA SABABU ZA KUGOMBEA UBUNGE

Wtaa wa sinema za Kibongo, Wastara Juma.
Na Gladness Mallya
BAADA ya hivi karibuni kutangaza nia ya kugombea ubunge wa Viti Maalum kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) huko Morogoro Vijijini alikozaliwa, staa wa sinema za Kibongo, Wastara Juma ameibuka na kueleza kwamba ameamua kufanya hivyo ili kuwatetea walemavu na watoto wa kike.
Akipiga stori na Ijumaa, Wastara alisema wananchi ambao ni walemavu wamekuwa hawatendewi haki katika maeneo mbalimbali kulingana na maumbile yao hivyo lengo lake kubwa ni kwenda kutetea haki zao ili ziwe sawa na watu wengine pamoja na sanaa kwani wasanii wamekuwa wakinyonywa kutokana na kazi zao kuuzwa hovyo.
Naamini nitashinda, kwani jimbo nililochagua mimi ni mzaliwa na nimekuwa mwakilishi wa akina mama na watoto kwa muda mrefu. Sasa ni wakati wa kwenda kuwawakilisha huko bungeni, alisema Wastara.

NISHA: KISIASA BADO NIPONIPO, NAENDA ZANGU CHINA KUTOA VICHEKESHO

Staa wa filamu za Kibongo, Salma Jabu ‘Nisha’ amesema kuwa hatarajii kugombea wala kujiingiza kwenye siasa kwa sababu bado yupoyupo katika eneo hilo.
Staa wa filamu za Kibongo, Salma Jabu ‘Nisha’.
Akizungumza na Ijumaa, Nisha alisema kuwa, katika kipindi hiki cha mikikimikiki ya siasa atakuwa nje ya nchi kwani anatarajia kwenda China mwezi huu alikoitwa kufanya vichekesho.
“Nimepata dili, nitakwenda China kwa ajili ya kufanya comedy (vichekesho), nimepata fursa lazima niitumie ipasavyo. Kuweka muvi zangu mtandaoni kumenisaidia sana hivyo kwenye mambo ya siasa bado niponipo sana,” alisema Nisha.

ALI KIBA KINGEREZA HAKIMSUMBUI KAMA DIAMOND PLATNUM ONA MEETING ZAKE.


Ali Kiba baada ya kuteuliwa mwakilishi kwenye kampeni ya kuzuia vifo vya tembo WildAid amekuwa akikutana na mabalozi wakiwemo wa Marekani na msanii mkubwa wa filamu marekani Lupita Nyongo pamoja na familia yake.Katika maongezi ameonekana mtulivu wa nje na ndani ya nafsi ishara tosha anakimudu kingereza.Huku akipunguza matabasamu mengi wakati wa maongezi kama timu pinzani. 


 


BONYEZA HAPA KUONA VIDEO ALI KIBA AKITEMA YAI BALAA

PICHA ZA KUMKASHIFU DIAMOND YASAMBAZWA MITANDAONI

AUNT EZEKEL : NITAMUUNGA MKONO WEMA SEPETU KATIKA SAFARI YAKE KUGOMBEA UBUNGE

 
Diva wa filamu Bongo ambaye kwa sasa ni mama wa mtoto mmoja anayetambulika kwa jina la Cookie, Aunt Ezekiel, amefungukia kuhakikisha anampa sapoti ya nguvu shosti wake, Wema Sepetu katika harakati zake za kuwania ubunge.

unt amesema kuwa pamoja na kwamba yeye hafahamu siasa hata kidogo na hatarajii kujiingiza huko, lakini anatambua Wema ameamua kutangaza nia ya kugombea, hivyo kama rafiki yake mkubwa atahakikisha anazunguka naye kila sehemu ili kumsaidia atimize ndoto zake za kuingia mjengoni na kuwatumikia wananchi wa Singida.

Kesi ya Gwajima Yapigwa Kalenda


MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu jana imeshindwa kumsomea maelezo ya awali Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima na wenzake wanaokabiliwa na kesi ya kutumia lugha ya matusi na kushindwa kuhifadhi silaha.
 
Kesi hiyo ilitajwa jana kwa ajili ya washitakiwa kusomewa maelezo ya awali lakini iliahirishwa kwa kuwa Hakimu Mkazi Wilfred Dyansobera anayesikiliza kesi hiyo hakuwepo mahakamani.
 
Hakimu Mkazi, Thomas Simba aliahirisha kesi hiyo hiyo Julai 20, mwaka huu kwa ajili ya washitakiwa hao kusomewa maelezo ya awali mbele ya Hakimu Dyansobera.
 
Mbali na Gwajima washitakiwa wengine, ni Mlinzi wake, George Mzava, Msaidizi wake, Yekonia Bihagaze (39) na Mchungaji Georgey Milulu (31) wanakabiliwa na shitaka la kukutwa na silaha pamoja na risasi kinyume cha sheria.
 
 Katika kesi ya kwanza namba 85, Gwajima anadaiwa kati ya Machi16 na 25, mwaka huu katika Viwanja vya Tanganyika Packers Wilaya ya Kinondoni Dar es Salaam alitoa lugha ya matusi dhidi ya Askofu wa Kanisa Katoliki Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo akimueleza Askofu kwamba ni mtoto, mpuuzi asiye na akili katika namna ya kwamba ingeleta uvunjifu wa amani. 
 
Katika kesi nyingine namba 84 , Gwajima anakabiliwa na mashitaka ya kushindwa kuhifadhi silaha na risasi jambo ambalo ni kinyume cha sheria ya uhifadhi wa silaha za moto. 
 
Anadaiwa kati ya Machi 27 na 29, mwaka huu, ndani ya Jiji na Mkoa wa Dar es Salaam, alishindwa kuhifadhi silaha aina ya Beretta namba CAT 5802, risasi 3 za pisto na risasi 17 za shotgun. 
 
Katika mashitaka mengine yanayowakabili washitakiwa wengine, inadaiwa Machi 29, mwaka huu katika Hospitali ya TMJ Mikocheni ‘A’ walikutwa wakimiliki silaha na risasi hizo bila ruhusa kutoka mamlaka husika.

Amuua Mwenzake Kwa Kisu Wakigombea Mwanamke


WATU watatu wamekufa katika matukio matatu tofauti katika Wilaya za Tarime na Rorya akiwemo mtu aliyeuawa wakati wanagombania mwanamke.
 
Waliokufa ni Chacha Mwita (24) aliyechomwa kisu kifuani na mwenzake wakigombea mwanamke wa baa huko Sirari. 
 
Wengine ni Juma Nguka (25) aliyeuawa na watu wenye hasira baada ya kutuhumiwa kupora pikipiki yenye namba za usajili MC 936 ACA, mali ya Erick Jumanne mkazi wa Kijiji cha Mkoma.
 
Tukio lingine ni kufa maji kwa mvuvi aliyefahamika kwa jina la Wambura Maregeri (30) mkazi wa kijiji cha Muhundwe aliyekufa maji baada ya Boya kutoboka.
 
Kaimu Kamanda wa Polisi Tarime Rorya ACP Swetbert Njewike alisema kuwa matukio hayo matatu ya vifo yalitokea Julai mosi mwaka huu katika Wilaya za Rorya na Tarime.
 
Akielezea tukio la baa ambalo Mwita aliuawa, alisema siku hiyo marehemu akiwa baa moja katika mji wa Sirari, Tarime, nyakati za saa moja jioni kulitokea ugomvi kati ya marehemu na mtu mwingine ambaye hajafahamika jina lake wakigombania mwanamke aliyetajwa kwa jina moja la Dina.
 
Alisema wakati wa ugomvi huo, Mwita alichomwa kisu kifuani na aliyefanya kitendo hicho alitoroka ambapo majeruhi huyo alitokwa damu nyingi na alipofikishwa Hospitali ya Wilaya Tarime alifariki dunia.
 
Alisema Nguka yeye alipoteza maisha baada ya kushambuliwa na wananchi wenye hasira baada ya kudaiwa kuiba pikipiki. 
  
Akasema Maregesi alikufa maji baada ya boya lililotengenezwa kienyeji alilokuwa anatumia katika uvuvi kutoboka na kuzama majini hali iliyopelekea kifo chake.
 
“Jeshi la Polisi linafanya msako wa watuhumiwa wa mauaji Chacha Mwita na watuhumiwa waliohusika katika mauaji ya Nguka ili waweze kufikishwa katika vyombo vya Sheria,” alisema.
 
Aliwaonya wananchi kutojichukulia sheria mikononi ya kuwauawa watu wengine badala yake wawafikishe katika vyombo husika vikiwemo vya Dola. 
  
 Aliwaomba raia wema kutoa taarifa mara watakapowaona watuhumiwa hao wa mauaji hayo ii wakamatwe.
© Copyright TUANGAZE BONGO
Back To Top