BEN POL AFUNGUKIA UHUSIANO WAKE NA MISS TANZANIA NAMBA 2, PART 1

03:27

Ben Pol katika pozi kwenye studio za Global TV Online.
MUZIKI wa Bongo Fleva unazidi kuchana mawingu kila kunavyokucha, ambapo ukizungumzia wasanii wanaotoa mchango mkubwa katika muziki huo ni vigumu sana katika ‘listi’ yako kumsahau mkali wa RnB, Benard Paul ‘Ben Pol’.
Alianza gemu mwaka 2010 baada ya kutoka na kibao cha Nikikupata, baada ya hapo amewika kwa vibao vikali vingi kama vile, Jikubali, Samboira, Pete, Sofia na wimbo wake mpya uitwao Ningefanyaje aliomshirikisha msanii kutoka nchini Kenya, Avril.
Hivi karibuni, Ben Pol alitembelea Ofisi za Global Publishers na kufanya mahojiano na Global TV kupitia Kipindi cha Mtu Kati ambapo katika makala haya anafunguka zaidi;
YUKO CHINI YA MENEJIMENTI?
“Hapana kwa sasa Ben Pol ni msanii anayejitegemea japo anafanya kazi na timu, yaani kuanzia booking za shoo, kolabo na shughuli zote za kimuziki.”Ben Pol aliongeza pia kuwa huko nyuma aliwahi kuwa katika menejimenti mbili ambazo ni Music Lab aliofanya nao ngoma nyingi zikiwemo Nikikupata na Maneno Maneno pia akajiunga na Pana Music ambao hajafanya nao wimbo hata mmoja hadi anawapiga chini.
Ben Pol na Mhariri wa Habari za Burudani GPL, Andrew Carlos katika pozi
KUHUSU UHUSIANO WA MAPENZI
Ben Pol anasema kwamba, kati ya vitu ambavyo vimekuwa vikimpa shida ni uhusiano wa mapenzi maana anakosa hata cha kuzungumza.“Kiukweli uhusiano wangu hauna ‘nyama’ kiasi hicho hadi nipate cha kuongea, niishie tu hapo nikiwa katika uhusiano sahihi nitakuwa huru kuzungumza.”
WASANII ANAOWAKUBALI BONGO
“Aisee, nawakubali wasanii wengi, lakini ninachoweza kusema wasanii wachache, Rama D ni mkali, Belle 9 ni noma maana ana sauti nzuri sana, Jux ni shida, mjanja na anaifahamu biashara ya muziki.”
UJIO WAKE MPYA
“Sasa nina ujio mpya mkononi unaitwa Ningefanyaje niliofanya na Avril, video yake nitashuti na Gorilla Film chini ya Prodyuza Justin Compos nchini Afrika Kusini lakini baada ya ujio huo nitatoa ngoma nyingine na Nameless.”
SIRI YA NGOMA ZAKE KUWA KALI
Ben Pol anasema kwamba siri kubwa ya ngoma zake kuwa kali ni jinsi anavyoumiza kichwa na kutumia muda mwingi akitunga tena kwa umakini mkubwa utadhani msanii chipukizi ambaye hajasikika.“Unajua mimi huwa natunga utadhani underground ndiyo maana kila wimbo ninaoutoa unaonekana ni mkali, hiyo ndiyo siri kubwa katika kazi yangu.”

You Might Also Like

0 comments

Popular Posts

Like us on Facebook

Flickr Images